Home » » PRO.MSOLA:WEKEZENI KATIKA ELIMU

PRO.MSOLA:WEKEZENI KATIKA ELIMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Prof. Msola: Wekezeni katika elimuMBUNGE wa Kilolo, Profesa Peter Msola, amewataka wananchi wa jimbo hilo kuwekeza katika elimu kwa kupeleka watoto shule ili kuondokana na janga la kukosa elimu.
Profesa Msola aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kilolo katika Kijiji cha Mwatasi, wakati wa ziara ya siku moja na kusisitiza umuhimu wa wazazi kuwaelimisha na kuwapatia watoto wao elimu.
Msola alisema kuna wazazi ambao wanashindwa kuwekeza katika elimu na kuwafanya watoto kukimbilia mijini ambako hukutana na maisha magumu ya kuombaomba kutokana na kutokuwa na elimu.
Alisema kuwa maendeleo miongoni mwa jamii yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na kiwango cha uwekezaji katika elimu, hivyo ni vyema jamii iwekeze katika sekta hiyo ili kujikwamua na umaskini uliopo na kupambana katika soko la ajira.
“Tukumbuke kwamba kuwekeza katika elimu ni mkakati wa muda mrefu unaohitaji dhamira, subira na kwamba matokeo yake huonekana baada ya muda mrefu wa uwekezaji na faida kwa wazazi mara baada ya mtoto kusoma na kuweza kumsaidia pindi azeekapo,” alisema Prof. Msola
Prof. Msola alisema Kilolo ina rasilimali nyingi zinazohitaji viongozi wabunifu watakaohakikisha zinatumika kwa faida ya wananchi.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa