Home » » NYALANDU AIFUTIA LESENI KAMPINI YA GMS ILIYOLALAMIKIWA NA MSIGWA

NYALANDU AIFUTIA LESENI KAMPINI YA GMS ILIYOLALAMIKIWA NA MSIGWA


WAZIRI WA mali asili na Utalii, Lazaro Nyalandu (pichani) ametangaza rasmi kuifutia leseni ya uwindaji nchini pamoja na kuifuta kabisa kampuni hiyo katika shughuli za utalii nchini Kampuni ya Uwindaji  Green Miles Safaris Limited (GMS)  kutokana na kukiuka sheria mbalimbali za uwindaji Wanyamapori.

Nyalandu ametangaza uamuzi huo leo mchana jijini  Dar es Salaam, kutokana na kuridhishwa na ushahidi kuhusu kampuni hiyo kufanya vitendo vya kuwatesa wanyama pori.

Kampuni ya “Green Miles Safaris Limited(GMS) ililalamikiwa kwa mara ya kwanza na Mbunge Iringa mjini ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa, Bungeni mjini Dodoma wakati akiwasilisha bajeti kivuli ya wizara hiyo ambapo katika ushahidi wake aliwasilisha na CD ambazo zilikuwa na matukio hayo.

GMS ilituhumiwa kuendesha uwindaji haramu ikiwamo kujeruhi wanyama, kuuwa wanyama wa jinsi ya kike, kuchezea watoto wa Pundamilia, mtoto akiwinda na kuua ndege aina tandawala weupe na weusi na matumizi ya silaha zisizo na sauti.

 Green Miles Safaris Limited, inamilikiwa na Mtanzania, Salum Awadh.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa