Home » » MSIGWA AWATETEA MADIWANI 'KUTAFUNA' FEDHA ZA SAFARI

MSIGWA AWATETEA MADIWANI 'KUTAFUNA' FEDHA ZA SAFARI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, amekanusha kauli iliyotolewa na baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwamba madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa hawakusafiri kwenda Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Saalam, Lindi na Mtwara kwa ajili ya kujifunza, badala yake waliishia kula fedha za safari.
Amesema kuna baadhi ya viongozi wa CCM, ambao hawajui kutofautisha chama na mambo ya serikali kwa sababu wanaingilia majukumu yasiyowahusu.

Tuhuma hizo zilikuja baada ya Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga, hivi karibuni, kutumia mkutano wa hadhara, eneo la Kihesa Sokoni, kumshinikiza Meya wa Manispaa ya Iringa akubali kwamba, madiwani hao hawakusafiri kwa ajili ya mafunzo na kwamba, walikula fedha, ambazo zilitakiwa zitumike katika safari hiyo.
Msigwa alisema kuna baadhi ya viongozi wa CCM mbali na kutojua kutofautisha mambo ya serikali na chama, wamekuwa wakivuka mipaka ya kazi zao.

“Tunajenga nchi yetu wote. CCM tumewabana kila kona. Ndiyo maana kwa sasa wanajaribu kutafuta njia ya kutokea,” alisema Msigwa.Alisema baraza la madiwani linajua vema kuwa madiwani walisafiri na kwamba, hata mkurugenzi wa manispaa anajua kama safari ilifanyika na mkuu wa mkoa aliweka baraka zake.

Msigwa alimshangaa meya wa manispaa hiyo kusimama jukwaani kwa kuchanganywa na mtu, ambaye hajui miiko ya kazi yake.

“Mimi kama mbunge, najua madiwani walisafiri na walikofikia. Hata mimi nilikuwa nisafiri nikiwa kama diwani. Lakini nilipata udhuru, sikuweza kusafiri. Madiwani walisafiri na basi aina ya Coaster.

Meya alisema hawezi kusafiri na basi la pamoja, badala yake alisafiri na gari yake mwenyewe,” alisema.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa