Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MAMLAKA ya
Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) wilayani Makete, imeokoa zaidi ya sh.
Bilioni 1.4 katika ujenzi na maboresho ya chuo hicho kwa kuwatumia
wanafunzi na walimu kujenga miundombinu ya chuo hicho.
Wanafunzi hao na walimu, walijenga mabweni na vyumba vya madarasa kama makandarasi wa ndani.
Mkurugenzi wa VETA mkoani Iringa, Monica Mbele, alisema kupitia wanafunzi, wameokoa gharama ya ujenzi na utengenezaji wa samani.
Monica ambaye
alizungumza na mwandishi wa habari hii kuhusu mafanikio ya VETA hivi
karibuni, alisema majengo yaliyojengwa yana kiwango cha juu, na samani
zinazotumika chuoni hapo zimetengenezwa na wanafunzi.
Alisema chuo hicho kwa sasa kinauwezo wa kupokea wanafunzi 320 ambao watasoma kwa awamu mbili, mchana na jioni.
Chanzo;Uhuru Online
0 comments:
Post a Comment