Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
ZAIDI ya wajasiriamali 700 waliopatiwa mafunzo ya kutengeneza
batiki, sabuni na keki wametakiwa kutumia elimu hiyo kwa vitendo ili
wajikwamue kimaisha na kuongeza pato la taifa.
Wito huo umetolewa juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Mjasiriamali Kwanza ya jijini Dar es Salaam inayoendesha mafunzo hayo,
Dk. Didas Lunyungu, katika semina iliyowahusisha wajasiriamali zaidi ya
700 wa Mkoa wa Iringa.
Dk. Lunyungu alisema lengo la semina kwa wajasirimali hao ni
kuwajengea uwezo wa kujitegemea kupitia kazi za mikono na malighafi
zinazowazunguka ili wainue vipato vyao na taifa.
“Hapa mna rasilimali za kutosha, hamuwezi kujikwamua kiuchumi bila ya
kupata mafunzo yatakayowawezesha kuziona fursa zilizowazunguka na
kuzitumia…nawaombeni elimu hii muitilie maanani,” alisema.
Dk. Lunyungu alisema kuwa Mkoa wa Iringa umezungukwa na aina
mbalimbali ya vyakula na malighafi hivyo ni jukumu la kila mwananchi
kutumia fursa zilizoko kujikomboa kiuchumi na kuleta maendeleo ya nchi.
Alifafanua kuwa mara baada ya washiriki hao kumaliza mafunzo, taasisi
hiyo itawasaidia kuunda vikundi na uongozi wake lengo likiwa kufanya
tathmini ya namna wajasirimalia hao watakavyotekeleza kwa vitendo
mafunzo hayo.
Dk. Lunyungu alisema katika mafunzo hayo wajasiriamali wamefahamu
kupamba, kutengeneza egg chop, karanga za mayai, clips, sambusa, mafuta
ya mgando, mishumaa nguo za batiki na vikoi.
Aliongeza pia kuwa wajasiriamali hao wamepata mafunzo ya ufugaji kuku, nyuki, kilimo cha Uyoga na usindikaji wa maziwa.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment