Home » » POLISI WAJIPANGA KUPUNGUZA AJALI

POLISI WAJIPANGA KUPUNGUZA AJALI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
JESHI la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa limeweka mikakati ya kupunguza ajali za barabarani zinazozidi kuongezeka kutokana na uzembe wa madereva wachache mkoani hapa.
Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake jana, Mkuu wa Usalama Barabarani, Kamanda Leopord Fungu, alisema ajali za barabarani limezidi kuongezeka na kuwataka madereva kuwa makini na kufuata sheria za barabarani bila shuruti.
Fungu alisema hatakuwa na mzaha kwa madereva wazembe hasa wanaotumia barabara kuu ya Iringa kwenda mikoani na wakibainika adhabu kali itachukuliwa dhidi yao ikiwemo faini pamoja na kifungo.
 Chaanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa