Home » » JUST IN: UPIGAJI KURA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA KALENGA UNAENDELEA KWA AMANI NA UTULIVU

JUST IN: UPIGAJI KURA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA KALENGA UNAENDELEA KWA AMANI NA UTULIVU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Baadhi ya Wanakijiji cha Kalenga A,kata ya Kalenga Iringa Vijijini mkoani Iringa wakiwa wamejitokeza mapema leo asubuhi kupiga kura kumchagua Mbunge wamtakae wa jimbo hilo la Kalenga.Uchaguzi Mdogo wa Jimbo hilo unafanyika leo,ambapo vyama Vitatu;CCM,CHADEMA na CHAUSTA vikiwa vimesimamisha wagombea wake katika uchaguzi huo unaotokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo,pia Waziri wa Fedha,Dk William Mgimwa.Aidha Wagombea wa Chadema Grace Tendega na wa CCM,Godfrey Mgimwa ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kuchuana na hatimaye mmoja wao kuibuka kinara kwa kupigiwa kura na Wananchi,huku mgombea wa CHAUSTA,Richard Minja akipewa nafasi ndogo kutokana na maandalizi hafifu ya ushiriki wake.
 Baadhi ya akina Mama waliojitokeza kupiga kura mapema leo asubuhi katika kijiji cha Kalenga A,kata ya Kalenga Iringa Vijijini wakitazama majina yao kwenye ukuta tayari kwa kutumia haki yao ya msingi ya kumchagua kiongozi wamtakae kwa kupiga kura
 Mmoja wakazi wa kijiji cha Mangalali,kata ya Ulanda akiwa ndani ya chumba cha kupigia kura akisubiri kupiga kura mapema leo asubui.
Wakazi wa kijiji cha Mangalali,kata ya Ulanda jimbo la Kalenga,wakiwa nje ya chumba cha kupigia kura mapema leo asubuhi.Kwa ujumla katika kata kadhaa ambako Globu ya Jamii imepita kumekuwepo na utulivu mkubwa,wapiga kura wamejitokeza kadiri ya uwezo wao bila kubugudhiwa na hali ya namna yoyote,huku Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa likiwa limejipanga vyema kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa katika uchaguzi huo Mdogo wa Ubunge jimbo la Kalenga.
Kwa hisani ya Jiachie Blog

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa