Home » » UONEZI ULIOKITHIRI: ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA WA BARABARANI ALAZIMISHA FINE YA BILA KOSA KATIKA BASI LA NEW FORCE LINALOTOKA MBEYA KWENDA DAR BILA KOSA LOLOTE!!

UONEZI ULIOKITHIRI: ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA WA BARABARANI ALAZIMISHA FINE YA BILA KOSA KATIKA BASI LA NEW FORCE LINALOTOKA MBEYA KWENDA DAR BILA KOSA LOLOTE!!

ABIRIA WAKIWA WANASHUKA BAADA YA KUONA ASKARI HUYO WA USALAMA WA BARABARANI KUMVUTA DEREVA NA KUMALIZANA NAE PEMBENI
ASKARI WA USALAMA WA BARABARANI AKIWA ANAPANDA KATIKA BASI BAADA YA ABIRIA KUMJIA JUU NA KUDAI KUWA AMEKOSEA, HAPA ALILIWA ANATOA ABIRIA NA KUWAPELEKA ENEO AMBAPO NDIPO MALIPO YASIYO HALALI YALIFANYIKA
ABIRIA WAKIWA WANAENDELA KUMZONGA TRAFIKI HUYO AMBAYE ALIONEKANA ANAKIBURI NA KULAZIMISHA DEREVA  AENDE KITUONI KWA AJILI YA KULIPIA
KONDACTA WA BASI LA NEW FORCE WA KWANZA KUSHOTO AKIWASIHI ABIRIA WAINGIE NDANI YA GARI NA KWENDA KULIPIA
ABIRIA WAKIWA WANAPANDA KATIKA BASI TAYARI KWA KWENDA KULIPIA FINE ISIYO YA UHALALI NA UHALISIA
HAPA NDANI TRAFIKI HUYO AKIWA ANAWALAZIMISHA ABIRIA KUINGIA NDANI YA GARI ALI KUELEKEA KITUO KIDOGO KULIPIA.

 MMOJA YA ABIRIA AKIJARIBU KUMUELEKEZA ASKARI WA USALAMA WA BARABARANI JUU YA JAMBO HILO LAKINI ALIKUWA HAELEWI
HAPA ABIRIA WAKIWA  WAMECHACHAMAA BAADA YA KUJIWA VIBAYA NA ASKARI HAO WA USALAMA WA BARABARANI.



HIZI NDIZO COPY ZA FAINI HIYO AMBAYO ASKARI WA USALAMA WA BARABARANI WALIKATAA KUTOA  RISITI
*********
Katika  hari ya sinto fahamu leo majira saa  tano na nusu maeneo ya Iringa limetokea tukio la kusikitisha ambapo Askari wa usalama wa Barabarani alilikamata Basi la abiria lililokuwa likitoka Mbeya kuelekea Dar es salaam.

Trafiki huyo aliyekamata Basi hilo lenye namba za usajili T111CLU kwa madai ya kwamba kuna mtu ametoa taarifa ya kwamba aliovatekiwa kwa vurugu , na kumtaka dereva alipe fine kwa kuwa kosa hilo ni uvunjifu wa sheria za barabarani.

Hali ilizidi kuwa tete zaidi baada ya askari huyo kuulizwa mtu aliye ovatekiwa yuko wapi na kushindwa kumtaja huku abiria wakiwa wamechachamaa kutaka kumjua kwa sababu mpaka wanakamatwa kulikuwa hakuna hata sehemu ambapo Dereva huyo alicheza Rafu yoyote ile.

Baada ya mzozo uliochukua takribani ya dakika tano huku abiria wakitaka kumjua aliye  toa  taarifa hizo na Trafiki huyo kuto taka kumtaja kwa madai ya kuwa mtu huyo hawezi kutajwa, aliamuru basi hilo lipelekwe mpaka kituo kidogo ili liweze kutozwa faini.

Kitendo hicho ambacho kilikuwa ni cha kionezi, kiliendelea na hali kuwa mbaya zaidi baada ya ya Askari yule wa usalama wa Barabarani kutoa kauli na kusema"Sasa wewe Dereva tumekukamata na upo na  abiria wako hapa sasa amua Moja unasikiliza Abiria wako au unalipa faini uendelee na safari?"  Na kuendelea kusema "abiria hawa wanashuka Dar es salaam wewe Utabaki babarani" kauli hiyo ya kitisho iliwashangaza mashuhuda, huku Trafiki mwengine pembeni akiwa ana wachimba mkwara waandishi wa habari waliofika eneo lile na alisikika akisema "Hata kama ni waandishi hamuwezi kufanya chochote" ilikuwa ni kauli ambayo yeye alizania ni ya Kitisho.

Baada ya Hapo mmoja wa askari wa usalama wa barabarani alimwita Dereva pamoja na Kondacta wake ili wapate kulipia pesa ambazo kimsingi hazikuwa na TIJA yoyote ya kulipwa kwa sababu kulikuwa hakuna Ushahidi wa kutosha kwamba ni kweli walikuwa wamefanya kosa na Abiria wote walikuwa hawajaona kitendo hicho.

Baada ya mzozo wa takribani dakika 10 Dereva aliamua kulipia Fine hiyo ya kiasi cha Shilingi za Kitanzania 30,000 ambapo pia Dereva huyo alikili kabisa kwamba risiti aliyopewa sio sahihi.

Hata hivyo Madereva wa mabasi wamekuwa wakilalamika kila wakati ya kwamba wamekuwa wakinyanyaswa sana kwamba wanapofika eneo la Ipogolo Trafiki huwa wakiwasimamisha na kuambiwa kwamba wamechezea rafu magari madogo na kulazimishwa kulipia faini wakati Gari husika ambalo limefanyiwa makosa likiwa halipo, Wahusika wa mabasi wameongezea kwa kusema kwamba hakuna uwiano wa kulipia faini hizo na kusema kwamba wanatakiwa kupewa risiti ya Njano na wanapewa Risiti nyeupe.

Swali ni Je hali hii katika eneo la Iringa hasa pale Ipogoro itaendelea mpaka Lini? na je wahusika wanalizungumziaje hili?

Mpaka Abiria wanaondoka eneo la Tukio waliendelea kulaani kitendo kilicho tokea.

NA IRINGA YETU BLOG







0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa