Home » » MTOTO WA AJABU AZALIWA AKIWA NA MACHO MATATU NA KICHWA MFANO WA UYOGA IRINGA

MTOTO WA AJABU AZALIWA AKIWA NA MACHO MATATU NA KICHWA MFANO WA UYOGA IRINGA

 mtoto  zawadi Godfrey Mwingune mwenye  siku 19 kama anavyoonekana akiwa na macho matatu na uvimbe mkubwa  katika paji lake la uso  huku  kichwani kukiwa  na nundu mfano  wa uyoga ambayo inatoa usaa mwingi
 Hivi  ndivyo mtato  zawadi anavyoonekana kichwa chake  uzito  wake ni  kg 4 na nusu alizaliwa hospitali ya kibena Njombe ni mwenyeji  wa Ikengeza Isimani mkoa  wa Iringa
 Hapa mtoto  zawadi akiwa amejipumzisha katika  kitanda
Wazazi  wa mtoto  Zawadi Gofrey Mwingune Bw Godfrey Mwingune (30) na mama wa mtoto huyo Mathar Kitago (28) wakimtazama mtoto  wao kwa huzuni mwingi kutokana na kukosa  fedha za matibabu kwa ajili ya kumsafirisha mtoto  huyo kwenda kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Taifa

HUJAFA  hujaumbika ,Mungu ana makusudi yake ni yeye  ni muweza  wa  yote kwani ndie  aliyeumba mbingu na nchi pamoja na viumbe wote  wasioonekana na  wanaoonekana  hivyo mwacheni Mungu aitwe Mungu,ni kauli ya wazazi  wa mtoto  Zawadi Godfrey Mwingune aliyezaliwa akiwa na macho matatu na kichwa mfano  wa uyoga.

Akizungumza na mtandao  huu  wa  www.francisgodwin.blogspot.com mama mzazi  wa mtoto  Zawadi Bi .Mathar Kitago (28) mzaliwa wa  kijiji cha Kidegembye Lupembe wilayani Njombe  mkoani Njombe  alisema  kuwa hadi sasa anamwachia Mungu ambae ndie amempa zawadi ya mtoto  huyo.

Kwani amesema  kuwa  ilikuwa ni  siku ya jumapili January 13 mwaka  huu aliposhikwa na uchungu na  kukimbizwa katika  kituo cha afya cha  Kidegembye ambako alichukuliwa na  kukimbizwa  Hospitali ya wilaya ya Njombe  Kibena kwa matibabu zaidi.

Hata hivyo  alisema baada ya  kufika katika Hospitali hiyo aliingizwa katika  chumba cha upasuaji na  kufanyiwa  upasuaji na kubahatika kupata mtoto  huyo japo kwa upande wake  aliogopa  sana baada ya  kuonyeshwa  mtoto  huyo ila alipiga moyo  konde kwa  kuwa ni damu yake .

Bi Mathar mwenye  idadi ya  watoto  watatu  sasa akiwemo  Zawadi anasema  kuwa mtoto  wa kwanza wa kiume ana miaka 9 na mtoto  wa  pili ni  wa kike ana miaka 4  na  wote  alijifungua vizuri bila  kufanyiwa  upasuaji kama ilivyotokea kwa mtoto  Zawadi.

Baba  wa  mtoto  huyo Bw Godfrey Mwingune ambae anategemea  kuendesha maisha yake kwa  kilimo anasema  kuwa yeye ni mzaliwa wa kijiji cha Ikengeza Isimani na kuwa baada ya  kupata mtoto huyo  wa ajabu aliamua  kurejea nyumbani kwa  wazazi wake Igengeza  Ismani  ili  kuwaonyesha  mtoto  huyo japo anatambua  kuwa mtoto  huyo ni zawadi  kutoka kwa Mungu na ndio  sababu ya  kumpata jina la Zawadi pia.

" Kweli  nilipomleta kwa  wazazi  kijijini nao  wamebaki  wakishangaa kuona mtoto  wa ajabu hivyo ila sasa tunafanyaje  yote ni mipango ya Mungu "

Mwingune  alisema  kuwa hali ya afya ya mtoto  huyo si nzuri kwani mbali ya kuzawali wa kilo 4 na nusu ila bado anatatizo la uvimbe katika paji lake la uso pia  kichwani kuna kovu kubwa ambalo ni kama ncha mbili hivi ambalo linatoa usaa mwingi na kuwa  jeraha hilo alizaliwa nalo  mbali na vituko  hivyo pia alisema  katika  jicho lake la  kushoto kwa  juu  kuna jicho la pili na kufanya  mtoto  huyo kuwa na macho matatu .

Alisema  kuwa  tayari mtoto  huyo amepata  kutibiwa  Hospitali ya  Kibena  Njombe na Hospitali ya  Rufaa Mbeya  ila  imeshindikana na  madaktari  wamemtaka amkimbize katika  Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu  zaidi ama nje ya Tanzania .

Hata  hivyo mzazi huyo anasema  kuwa kwa  sasa pesa ya haraka inayohitajika  ni kiasi cha Tsh. milioni 1.5 ili kumwezesha  kwenda  kuanza matibabu Muhimbili japo gharama  za matibabu  zinaweza  kuongezeka  zaidi wakati kwa upande wake hana uwezo wa kupata hata shilingi 100,000 na kuwapongeza  wakazi wa Isimani ambao  wamemchangia kiasi cha  shilingi 300,000.

Mtandao huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com unakuomba  wewe mdau na msamaria mwema popote pale  duniani iwapo umeguswa na upo tayari  kumsaidia chochote mtoto  Zawadi ili kuokoa maisha yake  kuweza  kujitokeza kuchangia  chochote kwa namba ya M-PESA 0754 026 299 au TIGO PESA 0712 750 199

Kwani kwa pamoja  tunaweza kunusuru maisha ya Mtoto  Zawadi 
na Francis Gowdwin






0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa