Home » » MAKUBWA HAYA : HIVI NDIVYO VITUKO VYA DIWANI ALIYEFUMANIWA IRINGA..SHUHUDIA HAPA

MAKUBWA HAYA : HIVI NDIVYO VITUKO VYA DIWANI ALIYEFUMANIWA IRINGA..SHUHUDIA HAPA


Diwani  Elia Mgwila aliyesimama
Mpiga  kura  akigonga mlango  wa diwani  bila mafanikio

Nyumba  ya aliyofumaniwa  diwani  huyo na mke wa mtu  hii hapa
Hapa ni nyumbani kwa  mheshimiwa mlango ukiwa umefungwa  huku ufunguo ukiwa nje
Mwananchi akitoka kumwona diwani huyo  bila mafanikio  leo


Kama ni kituko cha mwaka basi hiki  pia ni kituko cha aina yake pamoja na diwani wa kata ya Ifunda  jimbo la Kalenga  wilaya ya Iringa mkoani Iringa  Mheshimiwa Elia Mgwila  kufumaniwa na kukatwa  sikio moja na kung'olewa meno ila bado  diwani huyo ambae ni majeruhi ameendelea  kugoma katukatu kwenda  Hospital kutibiwa majeraha hayo.

Wakizungumza na mtandao huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com  kwa nyakati tofauti ndugu wa karibu  wa diwani huyo mpenda vya watu  wamesema kuwa mbali ya madiwani wenzake na  viongozi wa CCM kumshawishi kwenda  kutibiwa  ila amegoma katakata  kuwasikiliza .

Mbali ya  kuwagomea  ngudu na marafiki hao bado diwani huyo amegoma kwenda  kituo cha  polisi kufungua shitaka hilo na kudai kuwa  yote anamwachia mwenyezi Mungu  muumba wa mbingu na nchi na vyote vilivyopo duniani .

Wakati  diwani  huyo akigoma  kufika Hospital kutibiwa taarifa  zinadai  kuwa jeshi la  polisi  ambalo lilikuwa  likimshikilia bwana mwenye mke  aliyefumaniwa na diwani huyo mkazi  wa kijiji cha Ifunda kibaoni pamoja na mdogo  wake na mkewe  wameachiwa  huru na jeshi la polisi ambalo lilikuwa  likiwashikilia kwa  tukio hilo la kumjeruhi  diwani .

Huku  habari  za kipolisi  zikidai kuwa  watuhumiwa hao  wameachiwa  huru  kutokana na diwani huyo kugoma  kufungua kesi juu ya shambulio  hilo  la mwili.

Kwa Hisani ya Francis Godwin

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa