Home » » WAKULIMA WALALAMIKIA UJAZO WA LUMBESA

WAKULIMA WALALAMIKIA UJAZO WA LUMBESA




Na Oliver Richard, Iringa
WAKULIMA katika mikoa ya Iringa na Njombe, wameitaka Serikali kupitia Wakala wa Vipimo na Mizani nchini (WMA), kukomesha ujazo wa lumbesa. Wakulima hao waliitaka Serikali kutoa elimu mara kwa mara, kuhusu sheria ya mizani na vipimo, ili kuongeza uelewa katika kukabiliana na tatizo hilo.

Wakulima hao walikuwa wakitoa malalamiko hayo katika mafunzo yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA).

Wakulima hao walisema, ujazo usiozingatia vipimo umekuwa ni kikwazo kikubwa kwao, kwani wafanyabiashara wamekuwa wakiwapunja kutokana na kipimo hicho.

Fikiria Nyambo ni mkulima mkoani hapa, alisema endapo sheria ya mizani itafahamika vizuri kwa wafanyabiashara na wakulima tatizo la lumbesa litakwisha.

“Elimu pia itasaidia kupunguza dhuluma kwa wakulima, ambao wamekuwa wakifanya shughuli za kilimo pasipo kupata manufaa kutokana na lumbesa,” alisema.

“Pia Serikali imekuwa ikipoteza pato lake kutokana na magunia yanayotumiwa na baadhi ya wafanyabiashara hao, kuwa na ujazo mkubwa tofauti na kipimo halali,” alisema Wittnes. Mwinuka.

Kwa upande wake mbeba mizigo (kuli), katika soko kuu la Iringa, Juma Mgongolwa alisema mizigo inayofungwa kwa mtindo wa lumbesa, imekuwa ikidhoofisha afya zao na mara nyingine kusababisha gata vifo kwa vijana wanaofanya shughuli hiyo.

Chanzo: Mtanzania

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa