Home » » MTUHUMIWA WA MAUAJI WA DAUDI MWANGOSI AFIKISHWA TENA MAHAKAMANI LEO

MTUHUMIWA WA MAUAJI WA DAUDI MWANGOSI AFIKISHWA TENA MAHAKAMANI LEO


Mtuhumiwa Pacficus akipelekwqa mahakamani chini ya ulinzi mkali 

Mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten Daud Mwangosi leo amefikishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi ya Wilaya kujibu shitaka lilalomkabili.Huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari.



Akisomewa shitaka lake na mwendesha mashtaka wa serikali Mkuu lilian Ngilangwa , amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni askari mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) mkazi wa FFU Iringa, anakabiliwa na shitakala la mauaji ya makusudi.




Amesema mtuhumiwa huyo mnamo 02 Septemba mwaka huu katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa alimuua Daudi Mwangosi kwa makusudi kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai.




Mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya hakimu Mfawidhi ya Wilaya Dyness Lyimo mtuhumumiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haiwezi kusikiliza kesi za mauaji.




Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, kinakataza mtuhumiwa wa mauaji ya kukusudia kupewa dhamana.




Mtuhumiwa amerudishwa mahabusu kutokana na kesi yake kukosa dhamana kisheria na kesi hiyo imeahirishwa hadi 7 Novemba mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo.


Mtuhumiwa huyo aliletwa chini ya ulinzi mkali wa polisi kaitka gari la polisi lenye number za usajili PT 1467.

Huku waandishi wa habari wakizuiwa kupiga picha jambo lililosababishwa kusukumwa kwa mwandishi wa majira Elias Ally na mmoja wa Polisi hao.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa