Home » » PICHA ZAIDI ZA MWANDISHI ALIYEPIGWA BOMU HUKO IRINGA.. TUNAOMBA RADHI KWA PICHA MTAZO ONA HAPA

PICHA ZAIDI ZA MWANDISHI ALIYEPIGWA BOMU HUKO IRINGA.. TUNAOMBA RADHI KWA PICHA MTAZO ONA HAPA




 VURUGU kubwa zimezuka katika eneo la Nyororo wilayani Mufindi kati ya polisi na wafuasi wa Chadema, baada ya askari hao kusambaratisha mkutano wa chama hicho na kusababisha kifo cha mwandishi wa habari na watu kadhaa kujeruhiwa.
Mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daud Mwangosi anadaiwa kuuawa kwa bomu lililorushwa na polisi katika vurugu hizo.
Awali, inadaiwa kuwa mwandishi huyo alishambuliwa kwa marungu na Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), kabla ya bomu hilo kumjeruhi vibaya tumboni na kusababisha kifo chake.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio, alisema wakati mwandishi huyo akishambuliwa na polisi, mmoja wa askari wa jeshi hilo aliwazuia wenzake kuendelea kumpiga akiwaeleza kuwa anamfahamu kuwa ni mwandishi wa habari, huku akimkumbatia.
Shuhuda huyo alidai kwamba jitihada za askari huyo hazikusaidia, kwani baada ya kutupwa kwa bomu hilo lililosababisha utumbo wa mwandishi huyo kutoka nje, polisi huyo naye alijeruhiwa mguu.
Chanzo Vijimambo Blog

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa