Home » » CHAMA CHA CHADEMA CHAELEZEA KILICHOTOKEA SIKU YA TUKIO LA KUUWAWA KWA DAUDI MWANGOSI

CHAMA CHA CHADEMA CHAELEZEA KILICHOTOKEA SIKU YA TUKIO LA KUUWAWA KWA DAUDI MWANGOSI



Mkurugenzi Wa Mafunzo Taifa Benson Kigaila akielezea tukio lilivyokuwa kwa waandishi wa habari leo.
---
Na Francis Godwin, Iringa.
Ikiwa ni siku tano zimepita toka kuuwawa kwa mwandishi wa habari wa channel ten na mwenyekitiwa klabu ya waandishi wa habari Iringa Daudi mwangosi katika vurugu baina ya polisi na CHADEMA huko nyororo mafinga.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo kupitia viongozi wake Iringa wameongea na waandishi wa habari kuhusu kile kilichotokea.

Akiongea na waandishi wa habari Iringa leo Mkurugenzi wa mafunzo na operesheni ya Movement For Change Taifa Benson kigaila, ameeleza kuwa lengo kubwa la Chadema tarehe 2.09.2012 kule Nyororo walikuwa na lengo la kufungua matawi na kufanya vikao vya ndani na wanachama wao na sio kufanya mikutano ya hadhara kama inavyosemekana.

Aliendelea kuleleza kuwa wakiwa katika ufunguzi wa tawi katika ofis ya kata Nyororo Polisi wafika na kutangaza kuwa watawanyike na wakamueleza RCO kuwa wapo kwaajili ya kufungua tawi na kufanya kikao cha ndani na kwamba polisi wakiingilia ndio watakao kuwa wanachochea vurugu.

Aidha Kigaila ameongeza kuwa wakati huo huo wakifungua Tawi hilo vyama vingine kama CCM nchi nzima walikuwa wakifanya chaguzi katika ngazi za Wilaya lakini hawakuzuiwa kwa kile kinasemwa kuwa ni kuingilia zoezi la sensa.

Baada ya kufanikiwa kufungua tawi walitangaza kuwa wanaelekea ofisi ya kata ili wakafungue tawi lingine lakini alipoingia RPC Kamuhanda ndipo alipoagiza na kusema kuwa hakuna kuzindua tawi ni kutawanisha watu na kufunga mkutano” alisema Kigaila.

Wakati wakielekea katika ofisi ya kata Marehemu mwangosi alimueleza kigaila kuwa anawasiwasi alipokuwa akirekodi wengi wa polisi wanaonekana si wa Iringa jambo ambalo anaeleza kuwa ndicho chanzo kikuu cha kuuwawa kwake. Huku akihoji kuhusu kamera na laptop za marehemu kutoonekana na kutotolewa taarifa mpaka sasa.
Naye katibu mkuu wa Zanzibar Hamadi Yusufu akielezea maneno ya mwisho ya marehemu alisema kuwa marehemu alikuwa akilalamika kuwa wamwachie kwani yeye yuko kazini wasimuue kwani anatekeleza majukumu yake “ Jambo ambalo polisi hao hawakuliktilia maanani nakuendelea kumpiga mpaka umauti ulipomfika.

Aidha Hamadi ameeleza kuwa wao kama viongozi walikuwa katika tukio hilo wako tayari kutoa ushaidi mbele ya tume huru itakayoundwa na si Tume iliyoundwa na Jeshi la polisi au Waziri Nchimbi kwasababu kwa macho yao waliona polisi ambao wanasimamiwa na wizara yake wakitekeleza dhana hiyo.

Katibu wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) Deogratias Munishi ameeleza “Kuhusu kauli ya Msajili ya Vyama John Tendwa kuwa haina maana kwani alitegemea yeye kama mlezi wa vyama vya siasa angefika katika eneo la tukio ili aweze kuwa na ajionee hali halisi vyama anavyovilea yeye vikinyimwa fursa ya kufanya kazi zao kama vyama vya siasa”

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa